Katika Wilaya yetu ya Monduli ni wakati sasa ndani ya Idara ya Afya tubadilishe namna ya utoaji huduma Kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa mara wanapo kuja Hospitalini hapa kupata huduma za matibabu. Hii itaongeza ukarimu na faraja Kwa mgonjwa na kumfanya afurahie na kupendezwa na huduma hivyo kufanya apende kurudi kutibiwa katika Hospitali zetu mara anapopata changamoto ya kuugua.
DC Kiswaga ameyasema hayo Leo Sept. 18, 2024 alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Idara ya Afya yaliyobeba dhima ya "Huduma Kwa Wateja" yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Elhiazina Wilayani hapo.
Akizungumza katika mafunzo hayo DC Kiswaga amewataka watumishi hao mara baada ya mafunzo kutumia elimu waliyoipata kutoa huduma bora kwa Wateja ambao ni wagonjwa mara wanapofika kutibiwa hospitalini hapo na kwamba jambo hili lisiwe tu Kwa hospitali ya Wilaya bali katika hospitali, zahanati na vituo vyote vya Afya vilivyomo Wilayani humo.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya Dkt. George Kasibante amesema " Kama ulivyo agiza Katika kikao chako cha Sept. 10, 2024 kuwa tufanye mafunzo ya siku tatu (3) tumetekeleza na tunaamini mafunzo haya yataleta tija Kwa watumishi na Wateja wetu Kwa ujumla. " amesema Dkt. Kasibante
Aidha, amewashukuru TANDIA kupitia wawakilishi wake Bi. Regina Maria Margarete Meissner Ambaye ni Mwenyekiti na mwanzilishi wa TANDIA- Health and Education for Tanzania pamoja na Marie Charlotte Ewenodere, MD Mwenyekiti Msaidizi wa TANDIA Kwa kutoa pesa nyingi takribani milioni 430 kwa ajili ya kuisaidia Wilaya yetu ya Monduli katika masuala ya Afya.
Sambamba na shukrani hizo kwa TANDIA, Dkt. Kasibante amemshukuru kipekee Bi. Joyce ambaye amekuwa kiunganishi Kwa Monduli na shirika laTANDIA ambapo hadi sasa Monduli imejipatia jumla ya Milioni 430 kutoka kwa shirika hii ambazo zimetumika kusaidia ujenzi, ununuzi wa vifaa tiba na kuwapatia mafunzo watumishi wa Afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwa chachu Katika mafunzo haya kwa Idara ya Afya ili kukumbushana kutimiza wajibu wawapo kazini. Pia amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ambazo zimeboresha mazingira ya kazi, kwani sasa dawa zipo, vifaa tiba vipo, majengo bora yamejengwa, pamoja na magari Kwa ajili ya kubeba wagonjwa. Hivyo sisi watumishi wa Monduli tuna muahidi Mama tutafanya kazi kwa bidii na mafunzo haya yatakuwa chachu katika utendaji bora wa kazi.
Mhe. Kiswaga amewashukuru TANDIA Kwa kuunga mkono jitihada za Rais wetu Dkt. Samia za kuboresha Mazingira ya kazi Katika sekta ya Afya. Vilevile amewapongeza wawezeshaji wa mafunzo ya Huduma kwa wateja Dkt. Grayson Mhando na Dkt. Ladslaus kwa kutoa mafunzo hayo na kusema kuwa, kwa sasa tunahitaji huduma hii iboreshwe zaidi ili wagonjwa wetu wapate huduma bora.
Akihitimisha mafunzo hayo Mhe. DC Kiswaga amesisitiza kwamba, Kwa kuwa mafunzo haya yamefanyika kikamilifu Kwa makundi yote kutoka Vituo vya Afya, zahanati hadi Hospitali, " Nitaanza kufatilia ufanisi wa mafunzo haya." Amewashukuru tena TANDIA na kuwatunuku cheti kwani wameomyesha kutujali sana Wananchi wa Monduli nasi hatunabudi kuyaenzi mahusiano haya.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli