Akizungumza na wananchi Mhe.@joshua_nassari amesema kwamba Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania @samia_suluhu_hassan ametuletea maendeleo makubwa kwa kutuletea fedha nyingi hasa kwenye secta ya elimu hivyo basi tutunze raslimali hizi kwani ni hazina nzuri na bora kwa nchi yetu..
Aidha amewashukuru wanakijiji,Mwenyekiti pamoja na Diwani wa kata ya Monduli juu kwa usimamizi mzuri wa mradi huo tangu ulipoanza mpaka kufikia hatua ya mwisho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya monduli @isack_joseph_copriano amewataka na kuwaomba wananchi wa kata ya monduli juu na wanakijiji wa kijiji cha Emairrete kutunza shule hiyo kwa kupanda miti na kunzingatia uzio na mipaka ambayo inaonyesha mwanzo wa kiwanja ilipoanzia shule hiyo.asisitiza kuangalia mifugo kwa jamii ya kifugaji kuwa makini kwani eneo la shule ni kwajili ya kusoma hivyo basi wanafunzi kusoma kwa utulivu.
Vivyo hivyo,Diwani wa kata ya Monduli juu na Makamu mwenyekiti halmashauri ndug.Meiyan ametoa shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa wilaya ya monduli Joshua Nassari kwa kuwa nao bega kwa bega kwanzia pale wanapoanza ujenzi wa shule hiyo mpaka pale ilipokamilika,kwani ameacha mambo mengi na kusimamia ujenzi wa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya monduli amehitimisha kwa kusema kumalizika kwa shule ya msingi ya Emairete ndio mwanzo wa kujipanga kwa kueka uzio/fensi katika shule. hivyo basi achangisha wadau mbalimbali fedha kwaajili ya kujengea uzio shule iyo na kuaidi wananchi kwamba watakapoishia yeye atamalizia.
Imeandaliwa na kitengo cha mawasiliano serekalini
Monduli
#Kazi Iendelee
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli