Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli leo 18.3.2024.
Ambapo lengo la kikao hicho ni kufahamiana na watumishi wakiwemo wakuu wa vitengo kutoka kila idara Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Aidha,Mhe.Festo Kiswaga Mkuu wa Wilaya ya Monduli amesisitiza suala la utendaji kazi ikiwemo suala la ukusanyaji wa Mapato atasimama nalo sambamba lakini pia kwa watumishi watakao kuwa wazembe atasimama nao kikamilifu katika utendaji wakazi.kwani ameeeleza hatutakiwi kuwa na watumishi walevi wavivu wa kazi katika hilo ataisimama nao sambamba.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji Bi.Happiness Laizer ameeleza anaomba ushirikiano kusimama peke ake hawezi hivyo tusaidiane kwa hali na mali katika kila jambo.Vile vile pia amegusia swala la ukusanyaji wa Mapato kuwa watu wahakikishe wanapokwenda dukani kununua kitu wahakikishe wanaulizia risiti ili kuweza kujua nani analeseni na nani ambaye hana leseni kwa kufanya hivi itasaidia sana wafanya biashara kukata leseni.
"Nawapongeza wote kwa kipindi chote ambacho mmejitahidi katika kuendelea kusonga mbele katika suala la ukusanyaji wa mapato kwani Monduli kwa kiwango kikubwa inaendelea nimechukua wiki moja kukaa na kuangalia maeneo ya Monduli na kuendelea kuifahamu vizuri.Hata hivyo pongezi nyingi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutukumbuka kwa kututumia fedha kwaajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwani ameinua sana Serikali kwa ujumla.inafika pahali sisi tunapokea simu kwamba tumepokea fedha kiasi fulani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Monduli hakika tunashukuru sana Serikali yake."amesema Festo Mkuu waWilaya.
Hitimisho,mkuu wa Wilaya amesema amefanya kazi kwa mda wa miaka mitano hivyo sio mara yake ya kwanza.asmesisitiza ushirikiano wakutosha katika kuiendeleza kazi.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serekalini.
Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli