Mradi wa mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa Wilayani Monduli
Mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ni mradi ulipangwa kutekelezwa kwa miaka 5 amabo umelenga katika kugharimia vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Wilayani vilivyoibuliwa na wanajamii wa Monduli.
Mradi unatekelezwa katika Wilaya 3 za Monduli,Longido na Ngorongoro na pia mafanikio ya mradi huu katika Wilaya hizi 3 utasababisha kupanuka kwa mradi hadi Wilaya nyingine 12 za Tanzania.
Mradi huu utasaidia Wilaya na mipango ya Wilaya kuweza kusaidia jamii kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi na kusaidia kuinua shughuli za uzalishaji mali.
Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Mazingira na Maendeleo(IIED).
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ina mamlaka ya kusisimamia rasilimali za mradi kwa kushirikiana na shirika la Haki kazi catalyst na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF).
Mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi utekelezaji wake upo katika awamu 2.
KUPATA MAELEZO YA KINA KUHUSU MRADI WA MABADILIKO YA TABIANCHI bofya hapa
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli