Wajumbe wakamati ya siasa mkoa wa Arusha wakiongozwa na mwenyekiti CCM Mkoa,Loy Thomas Sabaya wamefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Monduli Shule mpya ya msingi Emairete iliyopo kata ya Monduli juu,Shule mpya ya Sekondari Lepuruko pamoja na mabweni ya shule ya sekondari Engutoto.Jana 11.3.2024.Ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM Wilaya ya Monduli.
Ambapo kamati ya siasa Mkoa Arusha yapongeza Wanachi wa Monduli kwa kujitolea kwenye miradi ya maendeleo.lakini pia kamati hiyo ya siasa imepongeza mradi wa Shule ya Msingi Emairete ya mradi wa boost 2023 kwa kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa madarasa mazuri na usimamizi mzuri wa mradi huo mpaka hapo walipofikia.
Vilevile pia,kamati ya siasa yaagiza kukamilika kwa ujenzi wa shule mpya ya Lepuruko ambapo wajumbe wakamati ya siasa wamemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa kukamilisha mradi huo mwezi aprili 30 2024 ili wanafunzi waanze kuingia darasani kuanza kusoma.
"Mradi huu uko nyuma ya wakati kulinganisha na muda wa utekelezaji wa mradi licha ya changamoto zinazojitokeza na kusababisha uchelewaji wa mradi hivyo uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya tuhakikishe tunakamilisha mradi huu ifikapo aprili 30"amesema Mwenyekiti Sabaya.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Monduli mhe. Festo Kiswaga ameaidi kutekeleza mamagizi ya timu nzima ya kamati ya siasa Mkoa kuwa atafwatilia na kuhakikisha mradi huo unakamilika kama maagizo yalivyotolewa
Mradi huo umejumuisha ujenzi wa jengo la utawala vyumba nane vya madarasa,ujenzi wa maabara,maktaba,kisima cha maji matundu ya vyoo pamoja na kichomea taka ambapo umegharimu milioni 692.2.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha mawasiliano Serekalini
Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli