Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi mbalimbali kutoka idara ya Afya, Elimu na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji Feb. 26 hadi 27, 2025 katika Ukumbi wa chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) Monduli, wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Manunuzi (Nest) yenye malengo manne muhimu ili kuboresha masuala ya manunuzi katika Idara na Vitengo vyao ndani ya Taasisi.
Akieleza malengo hayo Bi. Nuru Bazaar na mwenzake Eva Apolinari wamesema kuwa baada ya mafunzo hayo wanatarajia kila aliyeshiriki atakuwa amejengewa uwezo wa kinadharia na Vitendo kuhusu ununuzi wa umma, atatambua ufanyaji kazi katika ngazi za chini za Serikali za Mitaa, ataweza kutekeleza vyema majukumu kwa kuzingatia vyeo, mamlaka na wajibu katika ununuzi na ugavi sambamba na kuweza kuepusha migongano ya kimajukumu kulingana na mpangilio wa Kitaasisi katika ununuzi na ugavi.
Aidha Bi. Nuru Bazaar ametaja misingi ya ununuzi wa umma kuwa ni pamoja na kuwepo kwa usiri, maadili na uadilifu, uwajibikaji, ushindanaji kupitia Mfumo wa Nest pamoja na kuzingatia thamani ya fedha katika manunuzi
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli