Nyumba za halmashauri ya wilaya ya Monduli zinazojengwa na shirika la nyumba la taifa imeamriwa zigawanywe nusu kwa nusu. Mgawanyo wa nyumba hizi utakuwa nusu kwa nusu kwa maana kwamba nyumba kumi zitatakuwa mali ya Halmashauri na zingine kumi zilizobaki zitakuwa mali yashirika la nyumba la taifa (NHC).
Maamuzi hayo halifanyika wakati wa kikao cha pamoja cha NHC na halmashauri. Kulingana na Mkataba wa awali nyumba zote ishirini zingekuwa ni mali ya halmashauri, lakini kutokana na ukweli kuwa halmashauri haikuweza kulipia gharama yote ya ujenzi wa nyumaba hizi ikabidi kuwe na majadiliano ya namna ya umiliki.
Akiongea mbele ya kamati ya fedha utawala na mipango katika eneo zilipojengwa nyumba hizi Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Monduli alisitsitiza, “CC andika;kuanzia leo mpaka wetu uko hapa, huku juu ni halmashauri na huku chini ni NHC” akimaanisha ghorofa tatu zenye jumla ya nyumba kumi ni mali ya Halmashauri na zingine ghorofa tatu zenye jumla ya nyumba kumi zilizoko upande wa kusini zitakuwa mali ya NHC tangu siku hiyo ya tarehe 27/4/2018. Naye meneja wa NHC mkoa wa Arusha akasema kuwa halmashauri itakabidhiwa rasmi nyumba hizo mwezi july 2018 kwani kwa sasa mafundi bado wanamalizia kazi ya kuingiza umeme.
Kwa ujumla nyumba zote ishirini zilijengwa kwa takribani Tsh. bil 2.2 hiyo kwa mgawanyo huu halmashauri inapaswa kulipa Tsh. bil 1.1 kwa kipindi kisichozidi miaka mitano. Kwa mustakabali huu halmashari ya wilaya ya monduli inatakiwa kuhakikisha kila mwezi inatenga fedha kutoka katika vyanzo vyake vya ndani ili kulipa fedha hizi kwa NHC.
Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Monduli ilikwishalipa takribani Tsh mil 380 katika Tsh bil 1.1 hivyo kubakiwa na deni la Takribani Tsh.mil 720 ambazo ndizo fedha halisi zitakazolipwa kwa kipindi hiki kisichozidi miaka mitano kuazia sasa.
Imeandikwa na E.Msifuni
Afisa TEHAMA (W)
MONDULI.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli