Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Monduli leo amepambanua mikakati iliyowekwa ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona. Mkurugenzi alitaja mikakati hiyo wakati akifungua mafunzo kwa washiriki wa mfunzo ya kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto juu ya tahadhari dhidi ya janga lla virusi vya Corona.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya monduli Stephen Anderson Ulaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli inaendelea kutoa elimu kupitia kwa makundi mbalimbali yakimo yale ya viongozi wa kimila, viongozi wa dini mbalimbali, wafanya biashara, maofisa wa serikali katika ngazi zote kuanzi vijiji hadi ngazi ya wilaya.
Ndugu Ulaya alisema pia kuwa halmashauri imetenga vyumba maalumu kwa kila kituo cha kutolea huduma kwa ajili ya kuhifadhi washukiwa wa COVID19 pindi watakapobainika kuwepo. Pia taasisi zote za umma na binafsi pamoja na maeneo ya biashara ikiwemo masoko, maduka,nyumba za kuabudia, holeli na vituo vya mabasi vimeweka maji yanayotiririka na sabuni kwa ajili wananchi kunawa mikono kabla ya kupata huduma kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya ugonjwa hatari wa corona.
Mafunzo haya ya kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto juu ya tahadhari dhidi ya janga la virusi vya Corona yaliratibiwa na wawezeshaji kutoka wizara ya afya kwa kushirikiana na chama cha kitaaluma cha maafisa ustawi wajamii Tanzania. Washiriki wa mafunzo haya walikuwa ni wajumbe wa kamati ya mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ngazi ya wilaya.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli