Monduli ni miongoni mwa Halmashauri nufaika na mpango wa serikali wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,000 katika vituo shikizi vya shule za Msingi, vituo hivyo shikizi ni maeneo ya yanayo tumika kufundishia wanafunzi wa Elimu ya Awali hadi darasa la tatu wanao kaa mbali na shule Mama.
Katika mpango huo Monduli imetajwa kujengewa jumla ya Vituo shikizi sita ambavyo vitakua na Jumla ya Madarasa 12 ambayo kila moja itagharimu shilingi Milioni 20 na kufanya jumla ya gharama ya ujenzi kuwa milioni 240.
Lengo la vituo hivyo ni kuwapunguzia umbali wanafunzi wa shule za msingi wanaotembea mwendo mrefu kufuata huduma ya elimu. Mpaka sasa kuna jumla ya vituo shikizi 1,155 katika halmashauri 148 hapa nchini. Aidha imebainika kwamba Halmashauri 36 ambazo idadi kubwa ya Halmashauri hizo zipo katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Miji hazina havina vituo shikizi vya shule.
kupitia mpango huu, Serikali itajenga vyumba vya madarasa 3,000 katika vituo shikizi 970 ambapo jumla ya shilingi bilioni 60 zitatumika.Ujenzi huo utawezesha wanafunzi 135,000 kupata vymba vya madarasa bora na ukamilishaji wa ujenzi huo utakwenda sambamba na ununuzi wa madawati 45,000ambayo yatatumika na wanafunzi wote.
Jumla ya Halmashauri 143 zitafaidika na mpango huu katika mikoa yote 26 ya Tanzania bara. Mgawanyo wa vymba vya madarasa katika Halmashauri umezingatia vigezo vya; idadi ya madarasa iliyopo.
Imeandikwa na Kuchapishwa na
Obed Emmanuel
Ofisi ya TEHAMA Halmashauri ya Monduli
#Tamisemi
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli