Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe Happiness Raphael Laizer amewarai Watumishi pamoja na Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli kuonesha ushirikiano katika utendaji hasa katika ukusanyaji wa mapato pamoja na Usimamizi wa miradi ya Halmashauri.
Mhe. Happiness ametoa rai hiyo akizunguzma kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekua Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Ndugu Raphael Siumbu baada ya mabadiliko yaliyofanyika na Raisa wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan yaliohusisha Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Makatibu tawala.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe Isack Joseph amemkaribisha Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa kumuaidi ushirikiano dhabiti katika utendaji kazi huku akimshukuru Mkurugenzi anaemaliza muda wake Ndugu Siumbu Raphael kwa kazi kubwa aliyoifanya katika wilaya ya Monduli.
Aidha ametaja swala nyeti la mapato kuwa bado hairidhishi na kuahidi kuwa kwa kasi wanayo endelea nayo wanaamini katika kukua katika ukusanyaji huo wa mapato katika Halmashauri kwa kushirkiana na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi mpya pamoja na watumishi wote wa Halmashauri.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Monduli Mhe Willson Lengima amesema chama cha Mapinduzi kipo tayari kushirikiana na Viongozi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kuleta maendeleo wilayani monduli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Aliemaliza muda wake Ndugu Siumbu Raphael amewashukuru Watumishi wote wa Halmashauri pamoja na Viongozi wengine wanao salia akiwemo Mkurugenzi mpya mhe. Happiness Raphael Laizer, huku akiwahasa wate kwa umoja wao kufanya kazi kwa kuheshimu Mamlaka zote.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli