Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa Tsh. Milioni 400 fedha za ruzuku kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu. Kituo cha afya mto wa mbu ni moja ya vituo vya afya nchini vilivyonufaika na fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Kazi zinazofanyika ni pamoja na ukarabati na ujenzi wa majengo ambayo ni wodi ya wazazi (Maternity ward), Jengo linalojumuisha chumba cha upasuaji (Theater), X-ray, Ultra Sound na maabara, jengo ya kufulia (laundry), nyumba moja ya mtumishi na tanki la maji.
Mradi unasimamiwa na kamati ya Usimamizi, Manunuzi, Ujenzi na Mapokezi. Mradi uko katika hatua ya umaliziaji ambapo kamati ya usimamizi inatarajia kukamilisha na kukabidhi mradi huo kwa Halmashauri mnamo tarehe 30.05.2018 kwa ajili ya kuanza kutumika. Mpaka sasa fedha zilizotumika ni Tsh. 262,735,138/= na kiasi kilichobaki kwa ajili ya kumalizia mradi huu ni Tsh. 137,264,862/=.
Awali Halmashauri ilipeleka kiasi cha Tshs. Milioni 37 na mchango wa Wananchi ulikuwa Tshs. 2,500,000/= ambapo fedha hizo zilitumika katika hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho. Mkurugenzi Mtendaji (W) ameshatoa fedha kiasi cha Tsh. Milioni 2 kwa ajili ya kusaidia shughuli za ufuatiliaji na Usimamizi wa mradi huo kutokana na fedha zilizopokelewa kiasi cha Tshs. Mil 400 kutoelekezwa katika usimamizi.
Kutokana na mradi kutakiwa kutumia nguvu kazi zaidi kutoka kwa Wananchi, kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kutotii wito wa kujitolea nguvu kazi. Aidha wananchi ambao hawakutoa ushirikiano wa nguvu kazi ni pamoja na wanachi wa Kata za Mto wa Mbu, Majengo na Migungani.
Katika ziara ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri iliyofanyika katika eneo la mradi tarehe 12/5/2018, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli walishauri yafuatayo;
Ziara hii ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ilipitia pia miradi mingine ya maendeleo katika wilaya ya Monduli ambayo ni ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nanja, ujenzi wa madarasa mawili na ukarabati wa bweni katika shule ya sekondari ya Lowassa, ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Afya katika zahanati ya kijiji cha Arkatani na ujenzi wa mabweni katika shule ya msingi Manyara Ranch. Baadhi ya miradi hii ilikuwa kwenye hatua ya umaliziaji.
-------------------------------------MWISHO------------------------------
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli