• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Monduli District Council
Monduli District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Malengo
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Eneo la Utawala
      • Tarafa
      • Kata
      • Vijiji
    • Idara
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Idara ya Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwezekaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Onana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelezwa
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria ndogo
    • Mipango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIKUNDI 26 VYA WANAWAKE NA VIJANA MONDULI VYANUFAIKA NA TSH MILIONI 115 ZA HALMASHAURI.

Posted on: July 12th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta amekabidhi hati za malipo zenye thamani ya jumla ya Tsh millioni 115 kwa vikundi 26 vya wanawake na vijana wilayani Monduli . Fedha  hizo zinazotokana na asilimia 10 ya makusanya ya ndani ya Halmashauri. Tukio hili lilifanyika  katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli tarehe 12 Julai 2018.

Akizungumza katika hafla hii, Mhe. Kimanta alinza kwa kuwapongeza wale wote wanaorudisha mikopo kwa uaminifu. Aliwaelekeza maafisa maendeleo ya kata kuwa ni wajibu wao kuhamasisha na kuunda vikundi vya ujasiriamali ili wananchi watumie fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri. Hali kadhalika amevitaka vikundi vinavyonufaika na mikopo hii kuwa na ubunifu kwa kutumia soko lililopo Wilayani Monduli, akitoa mfano wa kushona na kuuza sare za shule, soko la nyama za kuku katika ‘camp sites’ zilizopo eneo la Mto Wa Mbu na kuanzisha vikundi vya utengenezaji na usambazaji wa mikate Monduli Mjini.

Hafla hii ilihudhuriwa pia na Mhe. Julius Kalanga(Mbunge) na Mhe. Isaac Joseph (Mwenyekiti wa Halmashauri).

Mhe. Mwnyekiti wa Halmashauri naye aliposimama, alianza kwa kuwapongeza akina mama kwa kuhamasika kuuunda vikundi kwa ajili ya kutumia fursa hii ya mikopo. Alisema akina mama wanaaminika na mara nyingi wamekuwa waaminifu kurudisha mikopo wanayopewa kwa muda unaohitajika. Mhe. Isaac aliwatahadharisha wahusika kuwa wanapochukua mikopo wafanye biashara wenyewe wasimpatie mtu mwingine kufanyia biashara au kufanyika kwa matumizi mengine.

Wanufaika wa mikopo

Kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya; Mhe. Mbuge wa Monduli alianza kwa kusisitiza kuwa katika tukio kubwa la namna ile madiwani wote wangepaswa kuwepo ili kushuhudia matunda ya kazi yao. Pia akapendekeza kuandaliwa kwa kongamano la elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili vijana nao wanufaike na mikopo hii kama ilivyo kwa akina mama.

Hali kadhalika Rose Mhina ambaye ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya wilaya ya monduli akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji (W) alisema,  changamoto kubwa Halmashauri inayokabiliana nayo ni; baadhi ya vikundi kutokuwa waaminifu kwa kubadili madhumuni ya mikopo waliyoomba na kufanya shughuli nyingine na kusababisha vikundu hivi kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati.

Vikundi vilivyopatiwa mikopo vinatoka kata za Engaruka, majengo, Monduli mjini, Lemooti, Engutoto, Migungani, Mto wa mbu, Moita, Meserani, Makuyuni, Lolksale na Selela. Kuna jumla ya vikudi 26 vyenye jumla ya wanachama 531.

Imeandikwa na;

E.Msifuni,

Afisa TEHAMA (W)

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2017
  • MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA MOITA November 30, 2017
  • TANGAZO LA KAZI (NAFASI ZA UDEREVA)-MARUDIO June 08, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGIA NA KIDATO CHA KWANZA 2020 MONDULI

    December 09, 2019
  • SIKU 3 ZAONGEZWA KWA AJILI YA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA

    October 15, 2019
  • MACHINJIO YA KISASA YAZINDULIWA MONDULI

    January 03, 2019
  • WARATIBU ELIMU KATA WAPATA PIKIPIKI MPYA - MONDULI

    October 11, 2018
  • Angalia zote

Maktaba ya Video

WANAWAKE WANUFAIKA NA MAMILIONI YA FEDHA KUTOKA HALMASHAURI- MONDULI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • EDWARD MORINGE SOKOINE
  • TAARIFA YA UPANDAJI MITI
  • Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
  • Mto Wa Mbu - Monduli ilivyonufaika na Tsh. Milion 400

Viunganishi linganifu

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya ajira ya Serikali
  • Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora
  • salary slip portal

Waliotembelea Kiulimwengu

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Monduli District Council

    Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli

    Namba ya simu: +255 - 27- 2538006

    simu ya mkononi:

    Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz

Mawsilano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Malalamiko
    • ramani ya eneo
    • Huduma zetu

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli