Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Mazingira Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli Ndg. Frediric James Mnahela Leo Sept. 21, 2024 amewaongoza Wananchi wa kata ya Engaruka Kijiji cha Irerendeni Katika zoezi la usafi ambapo Watanzania wote wanaadhimisha siku hii muhimu Duniani.
Akizungumza baada ya zoezi la usafi Ndg. Fredric Mnahela amesema, " suala la usafi ni la kila Mwananchi na hivyo kila Mwananchi siku zote ajenge tabia ya kufanya usafi katika mazingira yake anayoishi na Kwa mfanyabiashara pia afanye usafi katika maeneo yake ya biashara, na kwamba kuwepo na vihifadhia taka (dustbins) kabla taka hizo hazijapelekwa sehemu husika yaani dampo. " Amesema Fredric Mnahela
Afisa Mazingira Fredric ameongeza kusema kuwa tunapo yaweka mazingira yetu safi majumbani, kazini na sehemu za biashara inatusaidia kuepuka magonjwa ya mlipuko na hivyo Afya zetu zinakuwa salama kwa faida yetu wenyewe na kwa maendeleo ya nchi yetu.
Aidha, Ndg. Fredric ametoa shukrani za pekee Kwa shirika la Engaruka Community Initiative Organisation (ENCO) Kwa kutoa ushirikiano mkubwa Kwa kutupatia vihifadhia taka(dustbins) ambavyo vimetufaa sana leo Katika siku ya usafi Duniani.
Kwa upande wa Wananchi kata hiyo, wameshauri kuwepo na mzabuni ambaye ata ondoa taka hizo katika maeneo yao na kuzipeleka mahali husika yaani dampo na kwamba Kijiji tayari kimekwisha tenga ekari 5 kwa ajili ya dampo.
Sambamba na hayo Wananchi wa Engaruka wamefurahishwa na zoezi hilo kwani imekuwa ni chachu ya kuwakumbusha wajibu wao Katika suala la usafi na kwamba wako tayari kutoa tozo za usafi wa mazingira.
Ndg. Fredric amewasisitiza Wananchi hao kulipatia kipaumbele suala la usafi wa mazingira na kuwataka wajitokeze kwa wingi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kufanya usafi wa kina.
Amehitimisha kwa kutoa elimu ya mpiga kura na kuwasisitiza Wananchi kujiandikisha na kujitokeza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli