Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Gloriana Kimath ameongoza kikao kazi cha tathmini ya lishe kwa robo ya nne (Aprili–Juni) kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri hiyo leo Julai 31, 2025.
Katika kikao hicho, Mhe. Gloriana amempongeza Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa usimamizi bora uliowezesha matumizi ya fedha za lishe kufikia asilimia 100, pamoja na kuhakikisha Kata zote 20 zinachangia chakula cha kutosha mashuleni na kuendesha maadhimisho ya siku ya lishe katika kila vijiji.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe, Ndg. Michael Mhombo alieleza kuwa utekelezaji wa viashiria vya lishe umefikia asilimia 80, huku idara mtambuka zikiendelea kushirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha masuala ya Lishe yanakuwa sawasawa ndani ya Wilaya ya Monduli kwa makundi na rika hitajika.
Afisa Lishe kutoka Kituo cha Afya Mto wa Mbu, Bi. Adventina Nyambuya, amewaeleza watendaji wa kata kuhamasisha Jamii katika maeneo yao ili maadhimisho ya siku ya lishe yaweze kufanyika kila baada ya miezi mitatu, wiki ya pili ya mwezi husika, kwa kushirikisha wataalamu wa kata wote. huku akihimiza suala la utoaji wa elimu ya unyonyeshaji bora kwa jamii, kulingana na kaulimbiu ya mwaka huu.
Mhe. Kimath alihitimisha kikao kwa kuwataka watendaji wa kata ambazo hazijafanya vizuri katika masuala ya Lishe ili kuongeza juhudi na kufikia malengo yaliyowekwa.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli