Kutokana na changamaoto ya ukame inayoikumba wilaya ya Monduli na kusababisha kukosekana kwa maji ya kutosha kwa matumizi ya binadamu na mifugo Serikali imepeleka mabomba katika shule mpya ya Sekondari mswakini na nafkoni zilizopo wilayani humo yatakayo tumika kusambaza maji kilometa 30 katika maeneo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Joshua Nassari akikabidhi Mabomba hayo katika shule mpya ya sekondari mswakini amesema kuwa Serikali inatambua hali ya ukame inayo wakabili wananchi wa Monduli hivyo amesisitiza kuusimamia na kutunza mradi huo ili kuondokana na adha ya maji
Kwa upande wake meneja Ruwasa Mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph Makaidi Pamoja na Meneja Ruwasa wilaya ya monduli Mhandisi Naville Msaki wanaeleza mpango mkakati wa mradi huo mpaka utakapo kamilika
Nae mwenyeki wa kijiji cha Mswakini juu Laizer Emmanuel kwa niaba ya wanachi wake ameishukuru serikali kwa jitihada wanazo zifanya za kukabiliana na Ukame katika Wilaya hiyo
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli