Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Laban Kihongosi, ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Manyara, iliyoko wilayani Monduli, Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi milioni 174.7, ambapo Shilingi milioni 154.7 zimetolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya Tatu, huku wananchi wakichangia Shilingi milioni 20.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kihongosi amepongeza uongozi wa Wilaya pamoja na Wananchi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, huku akibainisha kuwa ubora wa kazi unaendana na thamani ya fedha za umma zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu Mkoani Arusha, ikiwemo ujenzi wa mabweni ya wavulana na wasichana ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na salama. " amesema Mhe. Kihongosi
Shule ya Sekondari Manyara ni miongoni mwa shule kongwe za serikali wilayani Monduli, iliyoanzishwa mwaka 1991. ambapo hadi sasa shule ina jumla ya wanafunzi 1,493, wakiwemo wasichana 778 na wavulana 715. Pia ina kitengo cha elimu maalum chenye wanafunzi 125, wakiwemo wavulana ni 38 na wasichana 87.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli