Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika leo, Juni 16, 2025, katika viwanja vya Kanisa la KKKT lililopo Monduli mjini, maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “ Haki za Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tunakokwenda.” yanalengo la kutoa elimu kuhusu haki za watoto na kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na unyanyasaji katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Festo Shem Kiswaga, Ndg. Muhsin Kassim ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo amewataka wazazi, walezi na wadau wote kushirikiana katika malezi na ulinzi wa watoto ili kujenga Taifa lenye maadili huku akisisitiza jamii kuungana katika kutokomeza ukatili wa watoto na tabia hatarishi zinazohatarisha ustawi wao
Katika maadhimisho hayo, watoto walipata nafasi ya kutoa burudani, kusoma mashairi, na kushiriki mijadala kuhusu masuala yanayowahusu, ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uelewa na ujasiri wa kujieleza katika jamii.
Ndg. Muhsin Kassim amehitimisha maadhimisho hayo kwa kuwahimiza watoto kuwa na nidhamu, kujilinda na kuthamini elimu kama njia ya kufanikisha ndoto zao. Ikiwa ni pamoja na kutoa rai kwa wananchi wote wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba,
2025.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli