Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Imepongezwa kwa Usimamizi thabiti wa Miradi.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu tawala Mkoa wa Arusha Ndugu Missaile Musa Albano akiwa katika ziara maalumu wilayani hapo kukagua baadhi ya miradi ya Maendeleo.
Awali akikagua mradi wa nyumba ya waalimu (Two in One) katika shule ya sekondari Mswakini iliyojengwa chini ya mradi wa SEQUIP na kugharimu Shilingi Mil.98 amewapongeza viongozi kwa Usimamizi wa mradi huo uliokamilika.
Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha nyumban hiyo inakabidhiwa ndani ya wiki mbili zijazo ambapo ni pamoja na Mradi wa Maji unaosimamiwa na Walaka wa maji vijijini RUWASA ambao una lenga kufikia katika shule hiyo ili kuruhusu wanafunzi kuanza masomo mwezi January 2024.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala Amefika kukagua mradi wa Shule mpya ya sekondari Lepurko Unaotekelezwa chini ya SEQUIP na kugharimu Zaidi ya Shilingi Mil.500 ambapo shule hiyo imefikia hatua ya umaliziaji.
Katika mradi huo Ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa Utakelezaji wa mradi huo kwa Viwango tajika na kwa wakati elekezi.
"Mimi naomba kwa mradi huu wa lepurko tuishie hapa lakini ningependa tu tukamilishe haya maeneo machache yalio baki, tails, maabara mi nawashukuru endeleni na kazi nzuri, kwa monduli mradi huu umewatoa kimasomaso" amesmema Musa katibu tawala.
Katibu Tawala Mkoa amekagua mradi wa Bweni katika shule ya sekondari ya wasichana Irkisongo unaotekelezwa chini ya Fedha za TASAF ambapo akiwa katika mradi huo pia ameelekeza ukamilike kwa wakati na kumtaka Mkurugenzi kufuatilia swala na Vitanda ili jengo hilo litumike mapema January 2024.
Hata hivyo, katika kuhitimisha zaiara yale amekagua Jengo jipya la maabara katika hospital ya wilaya ya monduli Ulianza kutumika siku za hivi karibu ambapo akiwa hapo amezungumza na baadhi ya watumishi wa idara ya afya walifika kumpokea Kiongozi huyo.
Akizungumza na watumishi hao amewapongeza kwa kuhamia katika jengo hilo huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufanikisha dhamira ya serikali ya awamu ya sita.
Amewataka watumishi hao kuto kua na hofu ya kusemea Changamoto wanazo kutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao ili Serikali ifahamu na kitafuta namna bora ya kutatua Changamoto hizo.
Ziara hiyo ya katibu tawala imefanikiwa kufika na kukagua Mradi wa Nyumba ya walimu Mswakini, Shule mpya ya Msingi Losimingori, Mradi wa Bweni Shule ya sekondari Irkisongo pamoja na Jengo la maabara ya katika hospitali ya wilaya na kuhitimisha ziara yake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri iliyopo katika Jengo jipya la Utawala.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli