Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya TAMISEMI imepanga kujenga vyumba bya madarasa 12,000 vitakavyo gharimu shilingi Bilioni 240 katika shule za sekondari katika halmashauri mbali mbali nchiniikiwa ni kujiandaa kuwapokea wanafuzi wa kidato cha kwanza watakao jiunga mwezi Januari 2022.
Ujenzi huo wa vyumba vya madarasa unatokana na mahitaji kulingana na idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujinga na kidato cha kwanzanmwaka 2022 ambapo Kulingana na mchanganuo huo wa serikali imetaja halmashauri ya willaya ya Monduli kuwa ni mongoni mwa halmashauri nufaika na mpango huo kwa kuonyesha kuwa ina uhitaji wa jumla ya madarasa 71 na tayari ina madarasa 35 na kuwa na pungufu ya madarasa 36 hivyo katika mgao itapata madarasa hayo 36 ambapo kila darasa litagarimu shilingi Million 20 na jumla yake itakua Milion 720.
Matokeo ya ufaulu kitaifa yanatofautiana kati ya halmashauri moja na nyingine kwa wastani wa ufaulu wa kitaifa wa asilimia 90 ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza januari 2022 ni 1,022,936 mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 20,535 ambayo hailingani na idaidi ya vyumba vya madarasa 8,535 vitakavyo achwa wazi Novemba, 2021 .
Vimba hivyo vya madarasa vinajengwa kupitia mpango wa Maendeleo kwa wastani wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19, serikali itajenga vyumba vyote vya madarasa vitakavyo hitajika kwajili ya kidato cha kwanza mwaka 2022.
Ukamilishaji wa madarasa hayo 12,000 utawawezesha wanafunzi 600,000 kupata vyumba vya kusomea na hivyo utaondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarsa kwa asilimia 100 katika sule za sekondari.
Imeandikwa na Kuchapishwa na
Obed Emmanuel
Ofisi ya TEHAMA Halmashauri ya Monduli
#TAMISEMI
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli