Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo S. Kiswaga ametoa tamko na maelekezo juu ya utatuzi wa malalamiko ya uvamizi wa eneo la malisho na uuzwaji wa viwanja Kata ya Moita iliyopo Wilayani Monduli.
Tamko na maelekezo hayo yametolewa Jan 29, 2025 na Mhe. Kiswaga katika eneo la viwanja vya mpira vya Moita Bwawani ambapo katika hatua za utatuzi wa mgogoro huo ameagiza kufutwa kwa taratibu zote zilizofanyika juu ya ardhi hiyo na kuagiza Sheria, kanuni na taratibu zifuatwe na mchakato uanze upya .
Sanjari na hilo Mhe.Festo Kiswaga amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya mapito ya mchakato wa ujenzi wa ofisi ya Kijiji na uuzaji wa viwanja katika Kata hiyo.
Mhe. Kiswaga amehitimisha kwa kuhimiza Wananchi wa Moita kuendelea na ushirikiano katika eneo la malisho kwa ajili ya kulishia mifugo kama zamani na kwamba waendelee kulinda na kutunza amani na upendo vilivyokuwepo na kazi iendelee.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli