Wakulima na wafugaji waliovamia Msitu wa Lendikinya unao husisha kata mbili Kata ya monduli Juu na kata ya Sepeko Wilayani Monduli wametakiwa kusitisha mara moja shughuli za kibinadamu katika msitu huo ikiwemo kilimo,ufugaji na makazi.
Katazo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Joshua Nassari alipofika kukagua hali ya msitu huo ulioko chini ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ambao siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa uvamizi mkubwa wa wakulima kutoka vijiji vya jirani ikiwemo kijiji cha lendikinya.
Akizungumza mbele ya wataalamu alio ambatana nao wakiwemo maafisa Maliasili kutoka halmashauri ya wilaya ya monduli pamoja na waataalamu wa TFS amewataka wawekezaji wawili walio tajwa kuhusika katika uwekezaji wa mashamba hayo Bw. LAANYUNI SOKOINE na Mwenzake aliejulikana kwa jina moja DUNI kufika ofisini kwakwe siku ya Juma mosi 25.november 2023.
“Hawa ndio wateja kwahivyo lazima tuanze kwanza na wateja wawili, hawaiwezekani hawa waili waisumbue wilaya nzima Msitu umetunzwa tangu mika mingi hapana! Hao wateja wawili wafike ofisini kwangu juma mosi tuanzie hapo kudhibiti ” amesema Nassari.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya monduli Bwana Adili Mwanga akielezea historia ya msitu huo amesema tangu Mwaka 1972 msitu huo ulikua mzuri mpaka kufikia mwaka 1983 ambapo tangu wakati huo msitu ulianza kuvamiwa sana na wananchi.
Amesema mnamo mwaka 1996 serikali ya wilaya kwa kushirikiana na vijiji ikaanzisha kampeni ya kuwaondoa wavamizi wote katika msitu huo na kufanikiwa kuondoa kaya takriban 650, mwaka 2003 uvamizi ukaanza tena ambapo mpaka sasa bado juhudi za kuwaondoa zinaendelea.
Mwandishi wetu. @obedemmanuel.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli