Hi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli leo August 1, 2025, ameiongozaTimu ya Menejimenti (CMT)ya Halmashauri hiyo katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 inayotekekezwa Wilayani humo kupitia vyanzo vya Serikali kuu, mapato ya ndani, Lanes, Wash, TASAF, Boost, Sequip, mfuko wa Jimbo na P4R.
Katika Ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo timu ya Menejimenti ya Halmashauri hiyo imefanikiwa kukagua jumla ya miradi 17 iliyopo kata za Lashaine, Engutoto, Meserani, Moita, Lepurko, Mswakini, Esilalei na Mto wa Mbu wilaya humo na kushauri namna bora itakayosaidia ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.
Miradi iliyotembelewa na timu hiyo ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ni pamoja na ujenzi wa vyoo, madarasa, Zahanati na miundombinu mbalimbali katika miradi hiyo.
Bi. Happiness R. Laizer amehimiza uwajibikaji, usimamizi makini, na ubora wa kazi ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wananchi wa Monduli na inakamilika kwa wakati.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli