Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Gloriana Julius Kimath leo Julai 8, 2025 amefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na vikundi vitakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru hapo Julai 10, 2025 .
Katika ziara hiyo Mhe. Gloriana ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, pamoja na Viongozi na wajumbe wa Kamati ya Mwenge.
Aidha, Mhe. Gloriana Kimath ameridhishwa na maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru huku akisisitiza wananchi, wadau na Watumishi wote kujitokeza kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na zaidi kuwepo katika maeneo ya miradi inayozinduliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru hatimaye kukesha pamoja katika viwanja vya Polisi - Monduli mjini.
Mwenge wa Uhuru Wilayani Monduli utakimbizwa umbali wa kilometa 151 na kuzindua, kuweka jiwe la msingi pamoja na kutembelea miradi yenye thamani ya Fedha za Kitanzania bilioni 3.5.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli