Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Festo Kiswaga amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya hiyo Mhe. Gloriana Kimath leo Julai 2, 2025.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na na kushuhudiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri hiyo, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini kutoka Wilayani humo.
Mhe. Festo Shem Kiswaga amempongeza Mhe. Gloriana Kimath kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo huku akimtakia kila la kheri katika utendaji kazi wake sambamba na kumtaka kuwa na ushirikiano mzuri na Wanamonduli ili kuendelea kuboresha Wilaya hiyo yenye historia nzuri kwa nchi yetu.
Kwa upande wake Mhe. Gloriana Kimath ameahidi kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake kwa kushirikiana kwa karibu na wadau wote katika kuwatumikia wananchi kwa Maendeleo ya Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli