Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe Fredrick Lowassa amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia suluhu Hassana kwa kuendelea kulikumbuka jimbo la Monduli katika maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, maji pamoja na huduma zingine za kijamii.
Mhe Lowassa amemshukuru Rais akizungumza kupitia kofia ya ugeni Rasmi katika maafali ya 57 ya wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Elimu ya sekondari na Astashahada ya Elimu ya msingi katika chuo cha ualimu Monduli, yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho.
Katika hatua nyingine Mhe Lowassa ametumia mkusanyiko huo kuwaomba waalimu kuendelea kutoa Elimu na juu ya adhari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanasababisha khali Ngumu ya maisha kwa watanzania hasa jamiii ya kifugaji.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe Thomas Meiyan akiwa ameambatana na Mgeni Rasmi amewahasawa wahitimu wote kuendelea kuyaenzi yale maadili waliyofundishwa shuleni na kuwa wazalendo katika maeneo ya kazi.
Kaa upande wale Mchungaji Goodluck loishiye Laizer wa kanisa la FPCT makamu Ambae pia ni mkamu askofu wa jimbo la arusha ametoa nasaha kwa upande wa wazazi na kuwataka wahitimu hao kuwa mfano mzuri katika jamii baada ya kumaliza Masomo yao.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli