Mwenge wa Uhuru 2022, utapokelewa katika halmashauri ya Monduli,tarehe 21.06.2022 -saa 12.00 asubuhi, kwenye viwanja vya Barafu Mto wa Mbu ukitokea Wilaya ya Karatu. Katika halmashauri ya Monduli, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Kilomita 181.6 na kutembelea jumla ya Miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.7 katika sekta Elimu, Afya, Maji, na Vijana. Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2022, utafanyika kwenye viwanja vya Bomani Monduli Mjini Wananchi wote tiitokeze kupokea, kukimbiza na kukesha na Mwenge wetu wa Uhuru 2022.Kauli Mbiu : "SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO, SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA"
Mwenge wa Uhuru oyeeeeeee!!!!
MWL. RICHARD NGODA
MRATIBU WA MWENGE
WILAYA YA MONDULI
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli