Halmashauri ya wilaya ya Monduli imetenga shilingi milioni 50 kutoka mapato ya ndai Kwajili ya kujenga zahanati ya slela Ranch iliyopo kata ya Selela wilaya ya Monduli.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe Isack Joseph akizunguzma na wanachi wa Kata ya Selela baada ya kufika kukagua eneo litakalo jengwa zahanati hiyo.
Amesema tayari Million 30 zimetengwa ikiwa ni hatua ya awali ya kuanza ujenzi wa zahanati hiyo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Selela Mhe Richard Paul amemshukuru mwenyekiti wa Halmashauri na Uongozi wa Halmashauri ya wilaya lwa mapngo huo huku akikiri kuwa eneo hilo lilikua uhitaji mkubwa wa zahanati kutokana na umbali wa zahanati katika kata hiyo.
Aidha Mganga mkuu wa wilaya ya Monduli Daktari Edward Lengai amesema kwa upande wao wamepokea na watajitahid kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo ili kukamilisha kaa wakati.
wananch wa Eneo hilo nao wameimshukuru Serikali kwa kuwakumbuka katika huduma hiyo ya zahanati wakiamini kuwa ujenzi huo utawakomboa sehemu kubwa.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli