Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, amefungua Maonesho ya 31 ya Kilimo na Ufugaji Kanda ya Kaskazini leo, Agosti 5, 2025, katika Viwanja vya Themi jijini Arusha.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Mhe. Sendiga amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 139 kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ili kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na kuwapunguzia wakulima utegemezi wa mvua.
Ameeleza kuwa bajeti ya umwagiliaji kitaifa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 46 mwaka 2021/22 hadi bilioni 403 mwaka huu, hatua iliyosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao, utoshelevu wa chakula, na kukuza uchumi wa wakulima.
Aidha, amebainisha kuwa Arusha imepokea bilioni 85.2, Kilimanjaro bilioni 39 na Manyara bilioni 15 kwa ajili ya miradi hiyo. Pia amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wakulima kupitia maonesho hayo, na kuagiza tathmini ya tija ya maonesho ifanyike kila mwaka.
Amehimiza pia kuwepo kwa takwimu za hali ya lishe na udumavu kwa mikoa hiyo msimu ujao wa maonesho, akionesha wasiwasi juu ya kiwango cha tatizo licha ya uzalishaji kuwa mkubwa.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli