Lengo la kuwepo kwenu hapa kwa siku tatu lilikuwa ni kuwakumbusha majukumu ya Tume katika uratibu, usimamizi na uendeshaji wa Uchaguzi; majukumu ambayo baada ya uteuzi wenu sasa mnao wajibu wa kutekeleza majukumu hayo kwa niaba ya Tume.
Hayo yamesemwa leo Augosti 6, 2025 na Ndg. Emmanuel Richard Mpongo (wa tatu kulia) Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Monduli wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata katika Jimbo hilo yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Ndg. Emmanuel Mpongo amesema kuwa katika mafunzo haya ya siku tatu mmepitishwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo mapya kwa mujibu wa Sheria mbili mpya yaani Sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2025 ambazo zinataja namna ya kushuguulikia maombi ya wanaoomba kupiga kura moja tu ya Rais nje ya vituo walivyojiandikishia, na namna ya kushuguulikia usimamizi wa kura zitakazopigwa kwenye magreza.
Aidha, Ndg. Mpongo amewaeleza wasimamizi wasaidizi hao kuwa jukumu lililopo mbele yao ni kwenda kutoa mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizii wa vituo na Makarani waongozaji wa wapiga kura ili kuwawezesha kusimamia zoezi la uchaguzi kwa Weledi na usahihi, huku akiwataka kuyatafsiri mafunzo hayo kwenye vikao na vyama vya siasa na kila jambo lifanyike kwa mujibu wa Sheria.
Ndg. Mpongo amewaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa suala la utunzaji wa Siri lizingatiwe kwa kuwa wamekula kiapo na ukiukaji wa kiapo hicho ni kutenda kosa kinyume cha Sheria ambapo watawajibika kwa kosa hilo.
Naye Ndg. Petro Mwashiuya (wa pili kushoto) Afisa uchaguzi Jimbo la Monduli ametoa pongezi kwa washiriki wa mafunzo hayo huku akiwataka kutunza nyaraka vizuri kwaajili ya rejea za baadae.
Kwa upande wake Bi. Catherine Terry mnufaika wa mafunzo hayo amesema kuwa ushiriki wao katika mafunzo hayo umewajengea uwezo wa kutambua wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuwafanya wakatoe mafunzo kwa Weledi kwa wasimamizi wa vituo kama walivyoelekezwa.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli