Kikao Hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Ambapo Madiwani kwa Pamoja wamepokea na kujadilia ajenda zote za kikao ikiwemo changamoto katika baadhi ya maeneo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Monduli.
Miongoni mwa changamoto zilizo jadiliwa ni pamoja na changamoto ya ukosefu wa huduma toshelevu ya Maji ya kunywa katika kata ya Monduli Mjini na kata nyingine ikiwemo kata ya lesimingori.
Kupitia kikao hicho meneja wa Awusa wilaya ya Monduli akijibu kuhusu changamoto ya Maji kata ya Monduli Mjini amesema licha ya changamoto ya awali ya kuharibika kwa mitambo ya maji na kurekebishwa hivi karibuni wamekumbana na changamoto hiyo hiyo kuharibikiwa na mitambo, huku akitoa Rai kwa wanachi kuwa watulivu kwani wapo katika hatua za mwisho kurekebisha.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri kupitia baraza hilo ameiagiza idara zote zinazohusika na maji Awusa na Ruwasa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu kutatua changamoto hiyo ya maji kwa kwa kuwa wabunifu na kupanga bajet itakayo tatua changamoto.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli