Kikao cha Kamati Mseto ya Lishe Wilaya ya Monduli kwa kipindi cha robo ya nne Aprili hadi Juni 2024//2025 kimefanyika leo Julai 21, 2025 katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri hiyo ambapo kamati hiyo imepokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za Lishe zilizofanyika katika kipindi cha robo hiyo kutoka katika idara na vitengo mtambuka.
Aidha, Bi. Namnyaki Laitetei Mkuu wa Divisheni ya Raslimali watu ameongoza Idara hizo mtambuka ambazo ni Afya, Elimu, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, pamoja na Maendeleo ya Jamii kuwasilisha taarifa hizo zenye lengo la kutathmini mafanikio yaliyofikiwa, changamoto zilizojitokeza, na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za lishe, hasa kwa makundi yenye uhitaji maalum kama watoto na wajawazito.
Ndg. Haruna Haji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Happiness R. Laizer amehitimisha kikao hicho kwa kuwataka Wajumbe wa kikao hicho kuendelea kuwa na ushirikiano baina ya sekta ili kufanikisha utekelezaji endelevu wa afua za lishe na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa maendeleo ya afya ya jamii.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli