Na Mwandishi Wetu
Obed Emmanuel.
Askari wa jeshi la akiba wametakiwa kutumia fursa za kazi zinazojitokeza na kuacha tabia ya kuchagua kazi baaada ya kuhitimu mafunzo ya jeshi hilo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Joshua Nasary akifunga mafunzo kwa askari hao yaliyofanyika kitarafa katika eneo la mafunzo kata ya meserani wilayani monduli .
Amesema vijana wengi wanao pata mafunzo hayo wamekua na tabia ya kuchagua kazi kulingana na mazingira, hali, malipo na sababu zingine.
katika hatua nyingine Mhe Nasari amewahasa vijana hao kutumia taaluma na stadi zao kutoa msaada katika jamii hasa yanapotokea majanga ya mbalimbali ikiwemo ya moto, na ajali.
Meja Emmanuel Shayo ni mshauri wa jeshi la akiba Wilaya pia amesema mpaka sasa Vijana 50 wamepata ajira kwenye kampuni ya Suma-JKT Guardsn a wengine wakiajiriwa katika makampuni mengiine huku akikiri kuwa changamoto wanayokutana nayo zaidi ni vijana hao kuchagua kazi.
Diwani wa kata ya meserani mhe Lotti Napara ameshuru kuwepo kwa vijana hao wazalendo katika kata yake kwani ni sehemu kubwa kusimamia usalama katika kata hiyo ambayo hivi karibuni imekua na mchanganyiko wa watu kutoka katika miji ya jiraani.
Nae katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Monduli Bi Rukia Mbasha akirai ushirikiano kati ya kamati ya ulinzi na usalama na Askari hao.
Mafunzo ya kujikumbusha kundi la kwanza la mwaka 2023 Yamefanyika katika Tarafa ya Kisongo, Kata ya Meserani.
Yamekuwa na Jumla ya Askari 80 (wanaume 71, wanawake 9).
Waliofanikiwa kumaliza ni Askari 65 (wanaume 60, wanawake 5)
Mafunzo hayo yametumia muda WA wiki 7 na masomo yaliyofundishwa ni toka JWTZ, polis, uhamiaji, zimamoto, Takukuru, pamoja na Mganga mkuu hospitali ya Wilaya.
#Tehama
#Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli