Idara ya Elimu msingi ya Halmashauri ya wilaya ya Monduli Imefanya kikao cha Tathimini ya mtihani wa utamirifu (Mock) Darasa la Saba mwaka 2023.
Katika kikao hicho cha Tathimini kilichoongozwa na Katibu tawala Wilaya ya Monduli Ndugu Kasimu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Joshua Nasari ameipongeza idara ya elimu na Halmashauri na shule kwa ujumla kwa matokeo mazuri ya mtihani huo mwaka 20203.
Aidha akitaja Tathimini la kikao hicho cha ameitaka idara hiyo kuendelea kufanya vikao vya Tadhimini kwa kila mtihani ili kufahamu changamoto zinazo sababisha ufaulu wa shule kushuka.
Amewata waalimu kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanaongeza bidii kuendeleza ufaulu katika shule na kuendelea kushikilia nafasi hiyo au kupanda zaidi ya wastan huo walio nao kwa sasa
kwa upande wake Afisa Elimu awali na msingi Mwl. Natang'aduaki Mollel amewapongeza waalimu wakuu wa shule zote zilizo fikia wastani wa ufaulu na kuifanya wilaya kushika nafasi ya pili kimkoa katika mtihani huo.
Aidha amewataka waalimu na waratibu elimu kata walioshindwa kufikia wastan kujitafakari na kuanza kuchukua hatua za haraka ili kufikia wawastan husika na kuifanikisha wilaya kufikia katika lengo/malengo walilojiwekea.
Amewataka kushirikiana na waalimu waliofikia wastan ili kufahamu mbinu mbadala walizotumia kufikia ufaulu huo tajika na kwenda kufanyia kazi ilikuweza kuongeza ufaulu katika shule zao hasa katika mtihani wa taifa mwaka 2023.
Hata hivyo katika kikao hicho cha Tathimini kilichohudhuriwa na waalimu wakuu wote na waratibu wa Mewaka ngazi ya shule pamoja na waratibu elimu kata pia nao wamepata nafasi ya kutoa maoni yao juu ya kile kinachotakiwa kufanyika ili kufikia hatua tajika ya ufaulu katika shule zao kiwilaya, mkoa na Taifa.
Waalimu walioongoza kwa ufaulu wametoa semina fupi kwa wale walioshindwa kufikia wastan ambapo miongoni mwa Mambo walio sisitiza ni waalimu kuwa karibu na wanafunzi, Walimu kumaliza Mtaala mapema ili kupata muda wa kufanya marudio pamoja na kuandaa mitihani ya mara kwa mara.
Kikao hicho cha Tathimini ya mtihani wa utamirifu Mock Darasa la Saba kimefanyika hii leo tarehe 21/07/2023 chini ya idara ya Elimu Msingi wilaya
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli