Wakazi wa Mto wa Mbu Wilayani Monduli wametakiwa kuwa wakarimu kwa wageni hasa watalii kwasababu eneo hilo ndio kitovu cha utalii.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango alipokuwa akizungumza na wananchi wa monduli katika kata ya Mto wa Mbu.
Amesema Sekta ya Utalii ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu, hivyo ni muhimu kuwakirimi watalii wanaokuja ili waweze kutamani kurudi tena.
Dkt. Mpango amesisitiza kuwa Monduli hasa eneo la Mto wa Mbu ndio lango la utalii kwa Mkoa hivyo lazima waweke mazingira mazuri yakuvutia watalii.
@monduli_dc
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli