Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Lepuruko na Kata ya Migungani B, ambapo Shule ya Sekondari Lepuruko iliyopo kata ya Lepuruko na Shule ya Sekondari Migungani kata ya Migungani Leo Septemba 24, 2024 zimekaguliwa.
Katika ziara hiyo Mhe. Kiswaga amebaini kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa haujaenda sawa sawa na muda uliopangwa kwani takribani mwezi sasa bado ujenzi huo uko hatua za awali.Aidha, Mhe. Kiswaga amewataka Waandishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kuongeza jitihada za uwajibikaji ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika Kwa wakati.Ameongeza kuwa katika miradi yote nguvu ya Wananchi pia inahitajika ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa kuchangia walau maji na mawe katika kata zote huku akimpongeza Mhe. Diwani wa Kata ya Migungani Kwa kuchangia Lori 12 za mawe. Mhe. Kiswaga ameeleza " Baada ya wiki mbili nitakuja kufanya ukaguzi tena ili nione kama niliyoyaongea yametekelezwa." amesema Kiswaga.
Kwa upande mwingine, DC Kiswaga amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi.Happiness R. Laizer kwa usimamizi mzuri katika Ujenzi wa shule ya Sekondari Migungani kwa hatua waliofikia kwani inaonyesha matumaini mazuri ya kukamilika Kwa mradi huo.
Akisisitiza katika jambo hilo la ujenzi, Mhe. Kiswaga amewataka mafundi wote kuwajibika ipasavyo na kukamilisha miradi kwa wakati si kwa kuzingatia muda tu waliopewa bali pia kwa kuzingatia ubora wa kazi na viwango vya ujenzi vinavyo tambulika na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais makini Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Kiswaga amehitimisha kwa kuwasihi Wananchi kuona umuhimu wa kijitoa kwa ajili ya maendeleo katika maeneo yao hasa katika masuala haya ya elimu kwa watoto, kwa maendeleo binafisi na Tanzania kwa ujumla.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli