Ninatumaini kazi hii mtaifanya kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuhakikisha chanjo hizi zinatolewa kwa wahitaji wote ndani ya Wilaya ya Monduli, nami sitamfumbia macho Mtaalamu yeyote atakayebainika kwenda kinyume na maelekezo ya utoaji chanjo hizi.
Hayo yamesemwa mapema leo Julai 16, 2025 na Mhe. Gloriana Julius Kimath mara baada ya kuzindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya Tatu moja ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa chanjo hiyo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan huko Mkoani Simiyu.
Akisoma taarifa ya zoezi la utoaji wa chanjo ya Kitaifa kwa mifugo Bi. Pamela Ijumba Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amesema kuwa; Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imepokea dozi 200,000 za chanjo ya Tatu moja (mdondo, ndui na mafua) kwa kuku, dozi 225,000 za chanjo ya homa ya mapafu kwa ngombe, hereni 20, 000 kwa ajili ya utambuzi wa ng'ombe, pamoja na hereni 20,000 kwa ajili ya utambuzi wa mbuzi na kindoo.
Aidha, Bi. Pamela amekiri kupokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo ikiwemo jozi 15 za gumboot, overall 15, automatic syringes 25, madeli ( cool boxes) 25, sindano 169 kwa ajili ya ng'ombe, sindano 139 kwa ajili ya mbuzi na kindoo na gloves boksi Moja (1) huku akieleza kuwa utaratibu wa utoaji wa chanjo hizi ni bure kwa chanjo ya Tatu moja ambapo wafugaji watatoa shilingi 500 tu kwa dozi ya chanjo ya ng'ombe na shilingi 300 kwa dozi ya mbuzi na kondoo.
Naye Ndg. Haruna Haji ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Biashara, viwanda na Uwekezaji kwa niaba ya Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, amesema kuwa kama Halmashauri tunakiri kupokea hivyo vifaa na wataalam wamejipanga kuhakikisha zoezi hili litafanyika kwa ufanisi mkubwa. Hivyo ninawaomba Wananchi wapokee chanjo hizi ili kazi iende sawa sawa.
Kwa upande wake Bi. Marselina Shangali (wa kwanza kulia) ambaye ni mmoja wa wafugaji wa kuku Wilayani Monduli ameeleza kuwa yeye awali alikuwa anafuga kuku pasipo kuzingatia chanjo na hivyo ufugaji wake haukuwa na tija kwani kuku wengi walikufa. Hivyo kupitia chanjo hizi ninatarajia kufuga kwa tija na ufugaji wangu utakuwa wa viwango.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli