Viongozi wa dini endeleeni kuhubiri upendo kwenye nyumba za ibada, ili kuendelea kuwa na malezi ya kimaadili kwakuwa Malezi hayo yatasaidia kupunguza ukatili majumbani.
Hayo yamesemwa Julai 31, 2025 na Mhe. Gloriana Kimath katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, alipokuwa akizidua rasmi mafunzo ya Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto (MTAKUWA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo yakilenga zaidi kutoa elimu kwa Jamii juu ya ukatili wa kijinsia kwa makundi hayo.
Akizungumza kwaniaba ya Mganga Mkuu Wilaya ya Monduli ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya afya lishe na ustawi wa jamii Ndg.Costantino Rahhi amesema lengo kubwa nikupitisha kamati ya MTAKUWA ili kufahamu nini wanapaswa kufanya kwenye majukumu yao ili kuweza kupambana na majanga ya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Monduli.
Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, ameeleza kuwa malezi yenye kufuata maadili, kanuni na taratibu ni nguzo muhimu ya kumjenga mtoto mwenye maono chanya kwa jamii yake hivyo tuwakeeni watoto kwa kuzingatia maadili mema yanayokubalika katika Jamii
Naye Ndg. Denis Mgiye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Arusha ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo, ametoa elimu kwa wajumbe wa kamati juu ya majukumu yao na namna bora ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli