Naibu katibu mkuu Dkt. Charles Msonde kutoka ofisi ya Rais Tamisemi amefanya ziara wilayani Monduli kwa lengo la kuzungumza na walimu wa Wilaya ya Monduli kwaajili ya kutoa majibu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu,Ikiwemo swala la upandaji wa madaraja kwa walimu ambao wamecheleweshwa kupanda vyeo,kubadilishiwa muundo cheo baada ya kujiendeleza kutoka hatua ya cheti kwenda stashahada/shahada ya kwanza katika fani ya ualimu.
Akizungumza kwenye kikao hicho kilichohudhuriwa na walimu kutoka Wilaya ya Monduli pia amezungumizia juu ya madeni ya walimu kama mapunjo ya walimu (AREAS) kwa wale waliopandishwa madaraja nakuchelewa kulipwa mshahara mpya ameeleza kuwa serikali imejipanga na imejidhatiti namna ya kulipa madeni hayo.
Halikadhalika kwa upande wa madeni ya uhamisho ameeleza kwa wakurugenzi utaratibu ulioekwa kwaajili yakulipa madeni ya fedha za uhamisho na madeni hayo yote yanaendelea kulipwa.
Sambamba na hilo pia amezungumza kwa walimu swala la KPI yaani (performance key indicator) ofisi ya elimu msingi na sekondari kufanya ziara kuangalia utendaji kazi za kila siku katika shule zetu.
"Napongeza jitahada zinazofanyika kwa usimamizi mzuri wa miradi lakini pia sambamba na hilo tuna upungufu wa walimu shule za Msingi naomba mtukumbuke ajira zinapotoka kwani tumeanzisha shule mpya karibu nane na zote ni shule za msingi hivyo inatulazimu tuchukue walimu shule za zamani kwakufanya hivyo tunaleta upungufu pia kwa shule za zamani"amesema Mkurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Laizer
Kwa upande wake Afisa elimu Mkoa Ndug.Abel Ntupwa ameshukuru ofisi ya Rais Tamisemi kufika Wilaya ya Monduli kwa lengo la kusikiliza changamoto za walimu na kwa kwa halmashauri ya Monduli ni nzuri haina tatizo.
Akihitimisha kikao hicho Dkt Msonde amewataka walimu kufanya utendaji kazi kwa makini na weledi ukizingatia walimu wamepewa dhamana ya kuwatunza na kuwalea pamoja na kuwafundisha watoto ili kutengeneza taifa Lililo bora.
Imeandaliwa na kitengo cha mawasiliano serikalini
Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli