Wananchi 52 wa kijiji cha jangwani ziwani kata ya Mto wa mbu Wilayani Mondili walio adhirika na mafuriko msimu wa Mvua ulio pita wamekabithiwa hati za viwanja vipya katika ploti G makuyuni.
Viwanja hivyo vimekabidhiwa tarehe 22/09/2021 na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe. Izack Copriano ambapo amewata wananchi hao kuyahama makazi yao ya zamani yalio adhiriwa na mafuriko na kuanza makazi mapya katika viwanja hivyo.
Katika hatua nyingine Mhe.Copriano amewasisitiza kwa kuwaomba wananchi hao wa Jangwani wahakikishe wanaendeleza viwanja hivyo vipya na kuhakikisha maeneo yale ya zamani yanaendelezwa kwa shughuli za kilimo cha kawaida.
Aidha ameweahakikishia wananchi hao kuwa yupo tayari kuwatembelea katika makazi hayo mapya baada tu ya kuanza ujenzi.
Naye diwani wa kata ya Mto wa mbu Mhe.Hussen Mungia ametumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyekiti wa halmashauri kwa kugawa viwanja hivyo kwani lilikua hitajio kubwa kwa wananchi wa eneo hilo na kumuahidi kuwa atahakikisha wanachi hao watahamia makazi hayo mapya.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wameushukuru Uongozi wa wilaya ya Monduli kwa kuwakabidhi viwanja hivyo vipya zaidi ya 52.
Imeandikwa na Kuchapishwa na
Obed Emmanuel
Ofisi ya TEHAMA Halmashauri ya Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli