• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Monduli District Council
Monduli District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Malengo
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Eneo la Utawala
      • Tarafa
      • Kata
      • Vijiji
    • Idara
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Idara ya Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwezekaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Onana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelezwa
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria ndogo
    • Mipango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WILAYA YA MONDULI IMEUNGANA NA RC MAKONDA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI MKOA WA ARUSHA

Posted on: February 15th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda ameongoza wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa huo katika kampeni maalum ya usafi wa mazingira na upandaji miti, iliyofanyika leo  Februari 15, 2025 katika Kata ya Ambureni, Halmashauri ya Meru. Tukio hilo limefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa, likilenga kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuhifadhi uoto wa asili.

Katika hotuba yake, Mhe. Makonda ametoa maagizo madhubuti kuhusu utunzaji wa miti na mazingira, akisisitiza kuwa mtu yeyote anayehitaji kukata mti atapaswa kupata kibali kutoka ofisi za halmashauri husika.

"Kuanzia sasa, hakuna mtu atakayekata mti kiholela. Yeyote anayehitaji kufanya hivyo lazima apate kibali kutoka ofisi za halmashauri. Hatutaki kuona miti inakatwa bila mpangilio na kusababisha uharibifu wa mazingira."

Aidha, ameongeza kuwa mtu yeyote anayefanya maombi ya kibali cha ujenzi ni lazima aonyeshe sehemu atakayopanda miti kama sehemu ya wajibu wake wa kuhifadhi mazingira.

"Hakuna kibali cha ujenzi kitakachotolewa bila mwombaji kuonyesha ni wapi atapanda miti. Tunataka kuhakikisha kuwa maendeleo ya miji na vijiji vyetu yanaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira."

Wananchi na viongozi waliohudhuria kampeni hiyo walishiriki zoezi la upandaji miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Ambureni, wakionesha mshikamano wa pamoja katika kuhakikisha mazingira yanabaki safi na salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC MONDULI AWAPONGEZA MADAKATRI BINGWA WA MAMA SAMIA

    May 17, 2025
  • ELIMU YA LISHE, AFYA NA MAZINGIRA PAMOJA NA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE IENDELEE KUTOLEWA- MONDULI.

    May 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA 3

    May 14, 2025
  • MAMALISHE 30 WAPATIWA MAJIKO YA NISHATI SAFI -MONDULI

    May 14, 2025
  • Angalia zote

Maktaba ya Video

UFUNDISHAJI WA SOMO LA HISABATI KWA VITENDO KWA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI MAZOEZI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • EDWARD MORINGE SOKOINE
  • TAARIFA YA UPANDAJI MITI
  • Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
  • Mto Wa Mbu - Monduli ilivyonufaika na Tsh. Milion 400

Viunganishi linganifu

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya ajira ya Serikali
  • Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora
  • salary slip portal
  • Tanzania Safari Channel

Waliotembelea Kiulimwengu

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Monduli District Council

    Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli

    Namba ya simu: +255 - 27- 2538006

    simu ya mkononi:

    Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz

Mawsilano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Malalamiko
    • ramani ya eneo
    • Huduma zetu

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli