Jumla ya Wateule wa Uongozi ngazi ya mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na wajumbe wa Halmashauri ya kijiji 337 walioshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 katika Kata za Engaruka, Selela, Mto wa Mbu, Majengo, Esilalei na Migungani katika Wilaya ya Monduli, ninawaasa kutekeleza Majukumu yenu mara baada ya kuapishwa na kutenda kazi zenu kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Novemba 29, 2024 na Ndg. Sembere Siloma ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha huduma za sheria katika Halmashauri hiyo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Monduli Bi. Happyness R. Laizer huku akiwapongeza washindi hao kwa kupata nafasi hizo za Uongozi.
Ndg. Siloma amewaeleza kuwa ambaye hayupo katika zoezi hili la kuapishwa hataruhusiwa kuanza rasmi majukumu yake mpaka atakapo apishwa mbele ya Mhe. Hakimu.
Aidha, amewawataka viongozi hao waliopata nafasi kuwaongoza wananchi katika maeneo yao kwa miaka mitano kuwa, mara baada ya kuapishwa na kuanza kazi rasmi kuhakikisha Wanafanya vikao vyote kama inavyoelekezwa ikiwemo mikutano mikuu ya vijiji, kusoma na kutoa taarifa za kila mwezi, kutoa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji sambamba na kusimamia na kuibua miradi ya maendeleo katika vijiji na Kata zao.
Naye Abrahamu Logolie Mwenyekiti Mteule wa Kijiji cha Engaruka juu kwa niaba ya wenzake, ametoa shukrani zake kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na watendaji wake wote kwa kuimarisha usalama na amani katika kipindi chote cha Uchaguzi huku akiwashukuru wananchi waliomchagua na kuwa ahidi kufanya kazi pamoja nao vizuri kwa maendeleo ya Jamii na Serikali kwa ujumla.
Ndg. Sembere Siloma amehitimisha kwa kusisitiza suala la uaminifu na uadilifu katika utendaji kazi katika kipindi chote cha miaka mitano.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli