Timu ya Hamasa kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefika Wilayani Monduli Desemba 7, 2024 na kufanya hamasa kwa Wananchi kwa kutoa elimu ya Mpiga Kura huku wakieleza makundi mbalimbali yanayohusika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpiga Kura.
Akiyataja makundi hayo Ndg. George Kashura ambaye ni Afisa Tawala Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, amesema kuwa wananchi wote waliopoteza kadi zao, waliohama majimbo yao ya Uchaguzi, Kata na ama Mikoa waliyojiandikishia katika chaguzi zilizopota, ambao kadi zao zimeharibika au hazisomeki, waliotimiza miaka 18, na ambao watatimiza miaka kumi 18 mwakani Oktoba, 2025; hao ndio wanapaswa kujiandikisha ama kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpiga kura zoezi linalotarajia kufanyika kuanzia Tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024.
Timu hiyo imefanikiwa kutoa elimu ya Mpiga kura katika Kata za Monduli Juu, Monduli Mjini na Makuyuni; ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Wananchi walioweza kujibu maswali ya papo kwa papo yahusuyo kujiandikisha huku walio na kadi zao za Mpiga kura tiyari wakisisitizwa kuzitumza vizuri ili zitumike mwakani Oktoba, 2025 kuwachagua Madiwani, Wabunge na Mhe. Rais.
Ndg. George amehitimisha hamasa hiyo kwa kuwaeleza wananchi wa Monduli kuwa Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni kuanzia Tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024.
Kaulimbiu: " Kujiandikisha kupiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli