Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli pamoja na Wataalam kutoka Idara mbalimbali Wilayani humo, Leo January 9, 2025 wamefika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa lengo la kujifunza juu ya ukusanyaji wa mapato, usafi wa Mazingira na udhibiti wa taka pamoja na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Akiwakaribisha kwa upendo na bashasha Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba Kisagala ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza amewaeleza Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalam kutoka Monduli kuwa Jiji la Mwanza ni Jiji la pili Kitaifa kwa kukusanya mapato hivyo kwa dhima ya lengo la ziara hii, wamechagua Jiji sahihi kujifunza kwako.
Naye Bi. Amina Nassoro Makilagi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana(Mwanza Jiji) ameeleza kuwa" Halmashauri ya Jiji la Mwanza ni Jiji la pili kwa kuongeza pato la Taifa kwani mara kwa mara limekuwa ni Jiji linalovuka malengo ya ukusanyaji wa mapato waliyojiwekea ambapo kwa sasa Halmashauri imejiwekea kukusanya jumla ya bilioni 31." amesema Bi. Amina Makilagi
Akiwasilisha wasilisho la Idara ya Usafi na Mazingira Ndg. Desderius Polle Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Mazingira amesema " shughuli za usafi zinafanywa na mawakala wa usafi walioingia mkataba na Jiji pia kwa kushirikisha Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla huku tukizingatia uwepo wa vifaa vya usafi na dustbins kila mahali; sambamba na kutumia gari la matangazo kuwakumbusha wananchi kufanya usafi katika Mazingira yao ikiwemo usafi wa kila Mwisho wa mwezi.
Aidha, Waheshimiwa Madiwani na Wataalam hao wamepata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambao umetoa fursa nyingi za ajira kwa vijana na Wanawake pamoja na kukuza uchumi wa Jiji hilo kwa kuuza mazao ya mradi huo.
Waheshimiwa Madiwani hao pamoja na Wataalam wamehitimisha ziara yao kwa kutembelea kisiwa cha Saanane kilichomo ndani ya ziwa Victoria ambako wamejionea vivutio mbalimbali ikiwemo mnyama Simba, pamoja na ndege wa aina mbalimbali akiwemo tausi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli