Afisa Uandikishaji Jimbo la Monduli Ndg. Emmanuel Richard Mpongo leo Desemba 3, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, ameongoza kikao cha Wadau wa Uchaguzi chenye dhima ya kuwataka Wadau hao kutoa elimu kwa Wananchi ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la Mpiga kura zoezi linalotarajia kuanza Desemba 11 hadi 17, 2024.
Akizungumza na Wadau hao ambao ni Viongozi wa Dini katika Madhehebu ya Kikristo na Kiislamu, Malaigwanani, Viongozi wa makundi ya Vijana, Viongozi wa makundi ya Wanawake pamoja na Viongozi wengine mbalimbali kutoka vyama vya Siasa; Ndg. Mpongo ameeleza umuhimu mkubwa uliopo katika kutoa elimu ya kujiandikisha katika daftari hilo kwakuwa wananchi wengi wanachanganya kati ya uandikishaji wa Daftari la Wakazi uliokwishafanyika na daftari la kudumu la Mpiga kura ambalo litatumika katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2024.
Aidha, Ndg. Mpongo amesema " wanaotakiwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la Mpiga kura ni pamoja na wananchi waliotimiza miaka 18 na wale ambao kufikia Oktoba, 2024 watakuwa wamefikisha miaka 18, waliohamia Monduli awali walikuwa wakiishi Mikoa au Wilaya nyingine, waliopoteza kadi zao, wenye kadi zilizoharibika au zisizo someka." amesema Ndg. Mpongo
Naye Ndg. Benjamin Kolla Mchungaji wa Makanisa ya Waadventista Wasabato (SDA) Monduli ameahadi kutoa ushirikiano mkubwa kwa kutoa elimu kwa washirika wake Wilayani humo ili washiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu huku.
Sambamba naye, Ndg. Isaack Copriano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli ameshauri viongozi wa Dini kupewa ujumbe sawa usio na mkanganyiko ili watangazapo wananchi waipate tofauti ya daftari la Wakazi na hili la kudumu la Mpiga kura huku akisema katika ziara zake atatoa hamasa hiyo ya kujiandikisha.
Kwa upande wake Ndg. Ahmed Said Kisanda ambaye ni Shehe wa Wilaya ya Monduli ameshauri kuwa, kwakuwa muda wa hamasa ni mfupi tupewe vipeperushi vingi ili watu wanapo kusanyika katika maeneo ya Ibada wapewe vipeperushi hivyo ili ujumbe uweze kusambaa kwa haraka kwa ajili ya kuweka ufanisi katika zoezi hili.
Ndg. Mpongo amehitimisha kwa kuwasisitiza Wadau hao kupitia kauli mbiu kwamba " Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi bora."
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli