Umoja wa Vijana chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Monduli wameendelea na ziara yao ya kata kwa kata Wilayani monduli ambapo wakiongozwa na Mwenyekiti wa jumuiya Ndugu Panieli tutunyo wamefika katika kata ya engruka.
Mapema baada ya kufika katika kata hiyo wamekagua baadhi ya miradi inayotelelezwa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwemo jengo la Maabara katika shule ya oldonyo lengai na ujenzi wa zahanati katika kata hiyo.
Ambapo katika ukaguzi wa miradi hiyo mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wilaya Ndugu Paniel Tutunyo ameonesha kuchukizwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa wito kwa wasimamizi kuongeza kasi na kutekeleza kwa wakati uliopangwa.
Aidha Tutunyo amewataka vijana wa uvccm kuwa na maadili mema katika jamii kwa kuwaheshimu wakubwa na wadogo pamoja na Viongozi wote katika jamii na kufanya kazi kwa bidii na kujituma..
Katika hatua nyingine amewata vijana kuendelea kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kupata mikopo ya 10% zinazotolewa na Halmashauri ili kujiendeleza kiuchumi. huku akiwahasa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati pindi watakapo pewa.
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Monduli Ndugu Nurdin makamba ametumia jukwaa hilo kuwaahasa vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika maeneo yao ili kuleta chachu ya Maendeleo kwa jamii.
Nae katibu hamasa wa jumuiya hiyo Ndugu Alais Esoto ameupongeza Uongozi wa kata ya Engaruka na Serikali kuu kwa ujumla kwa utekelezaji wa miradi, huku akiwataka vijana wa uvccm kusemea na kupaza sauti kwa Yale yanayotekelezwa na chama cha Mapinduzi CCM.
Awali akizunguzma katibu wa Uvccm kata Ndugu Thomas Lazaro amemuomba mwenyekiti wa jumuiya hiyo kufanikisha mradi wowote wa kiuchumi utakao wasaidia vijana wa kata hiyo akipendekeza mradi wa mashine ya kusaga ili kujikimu kiuchumi.
Hata hivyo, mkutano huo umehudhuriwa na diwani wa kata hiyo ambapo ametolea maelezo baadhi ya changamoto zilizobainishwa na vijana ikiwemo mikopo ya Halmashauri ambapo amesema mpka sasa kasi ya ugawaji wa mikopo hiyo kwa kata ya Engaruka inaridhisha licha ya kuwa vijana wengi bado wanahitaji zaidi.
Na Obed Emmanuel
#UVCCMmonduli
#TEHAMA
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli