Leo Jumamosi Tarehe 29 Machi 2024 Katibu Tawala wilaya ya Monduli Mukhsin Kassimu kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga amepokea Timu ya Msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid ambayo imefika wilayani Monduli kutoa huduma za msaada wa kisheria bure kwa wananchi kusikilizwa na kutatuliwa migogoro mbalimbali ya kisheria.
Hata hivyo Bw. Khasim katika mazungumzo yake baada ya mapokezi ya wanasheria hao, amewataka wananchi wa wilaya ya Monduli kuchangamkia fursa hiyo ya Msaada kisheria ambayo itazuru kata 10 na vijiji 30 za Halmashari ya wilaya ya Monduli na kusema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa zaidi na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Naye Mratibu wa kampeni hiyo kwa Halmashauri ya wilaya ya Monduli kutoka wizara ya Katiba na Sheria Wakili Tunsubilege Boniface amesema timu hiyo siku ya leo itaanza kusikiliza kero kwa kata ya Monduli Juu na kesho Tarehe 30 machi 2024 itafika kata ya mto wa mbu, akiwataka wananchi kupashana habari hizi njema ili watu wengi wanufaike na msaada huu wa kisheria.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli