Shehena ya mabomba hayo yamepokelewa kijiji cha Mti mmoja na Mkuu wa Wilaya ya Monduli mhe.Festo Kiswaga kwa ajili ya usambazaji wa maji kwenye vijiji 13 ambapo kupitia mradi huo unao jegwa unazalisha maji milion 6 kwa siku na wananchi 60000 (elfu sitini)kutoka katika vijiji hivyo vilivyopo wilaya ya Monduli.
Kwa upande wake Mhe mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amemshukuru waziri wa Maji Juma Aweso kwa kuwajali wakazi wa wilaya ya Monduli katika secta ya maji kwani Monduli inaendelea vizuri.
Lakini pia mbunge amewataka wakandarasi waliosaini mkataba kwa ajili ya kazi hiyo kutendea haki mkataba wao kwa kufanya kazi kwa wakati ili kuweza kukamilisha ili wananchi wanufaike nahuduma ya maji,mhe.Fred amesisitiza nilazima kutendea haki mkataba wao wasipofanya hivyo kwa upande wake ataeka kazi yake matatani.
Vivyo hivyo Mbunge Fredrick Lowassa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Festo Kiswaga wamempongeza meneja ruwasa Monduli ndug. Msaki, kwa utendaji wake wa kazi mzuri kwa weledi kwani ametimiza wajibu wake ipasavyo kwa kila mradi kwani kwa upande wa miradi ya Monduli umeisimamia vizuri Monduli ni Injinia Msaki ni mfano wa kuigwa anaeitwa kwa wakati kwenye mradi na kwenda lakini pia kujitahidi kukamilisha miradi kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Monduli amemshukuru Mwenyekiti wa kijiji cha Mti mmoja kutoa eneo la heka 2.6 kwaajili ya sehemu yakujenga mradi wa maji lakini pia sehemu ya kuhifadhi mabomba ya maji.
"Wakandarasi imiliopewa kazi kamilisheni mradi kwa wakati sitokuwa na huruma na yeyote atakae cheza na fedha za serikali hapa mtakutana na chuma cha pua"amesema DC Festo.
Hitimisho,mkuu wa wilaya ya Monduli mhe.Festo kiswaga ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapendelea wananchi wa Monduli kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo lakini pia amempongeza Mhe.Mbuge wa Monduli Frederick Lowassa kwani ni mbunge asiesikika kwenye majukwaa Bali anafanya kazi nyingi kwa vitendo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli