Katika mkutano na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Iddi Hassan Kimanta kabala ya kupokea zawadi ya shuka la kimasai, rungu na pembe mbili za ng’ombe kutoka kwa Katibu Taarafa ya Kisongo Ndugu Paul Kiteleki, RC amewashukuru watumishi na wananchi wa Wilaya ya Monduli kwa ushirikiano waliompatia pindi alipokuwa Mkuu wa wilaya hiyo. Kimanta alisema kuwa sio juhudi wala ujanja wake uliomfanya apate nafasi hiyo bali ni ushirikiano aliyopata kwa watumishi wenzake pamoja na kumtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo.
Mkuu wa mkoa amesema anamshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dt. John Pombe Magufuli kwa kumteua yeye mwana Arusha kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha. Hali kadhalika amemtaka Mkuu wa wilaya ya Monduli Kamishna msaidizi wa Polisi Edward Jonatham Balele kufanya kazi kwa kushirikiana na watu. RC ameyasema hayo wakati akimtambulisha Mkuu huyo wa Wilya ya Monduli kwa wafanyakazi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Kimanta aligusia pia suala la usimamizi wa fedha za ujezi wa miundombinu ya shule kiasi cha shilingi Milioni 400 zilizochangwa na wananchi wa wilaya ya Monduli kuwa zisimamiwe vizuri. Alisema kuwa wakati atakapofanya ziara wilayani hapa ataanza na ukaguzi wa shule zote kuona utekelezaji wa mradi huo. Hivyo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli Ndg, Stephen Ulaya asimamie utekelezaji mapema iwezekanavyo.
Mheshimiwa Iddi Kimanta amekuwa mkuu wa wilaya ya Monduli tangu Mwaka 2016 hadi juni 2020 alipoteuliwa tena kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. uteuzi wa mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha uliambatana na uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mkuu wa wilaya ya Arusha na Mkururugenzi mtendaji wa jiji la Arusha.
E. msifuni.
A/TEHAMA
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli