Ras Mkoa amepongeza Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya fedha za umma pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Amesema katibu tawala mkoa kwa halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa miaka mitatu (3) mfululizo wamepata hati inayoridhisha kwamba matokeo haya yametokana kwakueka hoja zote sawa na kuepuka hoja zisizo kuwa za msingi.lakini pia pongezi za dhati kwa kujibu hoja zote vizuri na kuibua hoja nzuri za msingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Isack Joseph Copriano amesema kuwa hoja zote zimepitiwa na wajumbe kwa kushirikiana na wataalamu kwenye vikao vya kisheria na kwa mwaka huu,asilimia kubwa hoja zimefungwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo halmashauri ilikuwa na hoja kati ya 160 mpaka 180 hoja ambazo hazijafugwa.
"Ushirikiano uliopo baina ya madiwani na wataalamu wa ngazi zote wameendelea kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha hoja zote za ukaguzi,zinafanyiwa kazi kwa kuzingatia vigezo na hadi kufikia hoja 8 kutoka hoja kati ya 160 mpaka 180 kipindi cha nyuma"amesema mwenyekiti wa halmashauri Isack Joseph.
Vivyo hivyo Mwenyekiti wa halmashauri amempongeza Mkurugenzi Mtendaji bi.Happiness Laizer kwa kuwa msitari wa mbele kwa usimamizi mzuri wa mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwani hatua nzuri ya kuridhisha katika ukusanyaji wa mapato lakini pia kwakuwa naushirikiano mzuri wa uthubutu wa kushirikisha kila jambo hasa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
"Tulikuwa na hali mbaya Sana lakini kwa mwaka 2022/2023 halimashauri yetu ina hoja nane tu (8) ambazo ziko kwenye hatua za utekelezaji na tunategemea mwaka ujao wa fedha kufikia sifuri"amesema mhe.Isack mwenyekiti halimashauri.
Mwisho,mhe.isack Joseph ameshukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa inayofanywa kwenye wilaya ya Monduli kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile maji,afya,barabara,Elimu,Pamoja na utawala,miradi ambayo imerahishisha upatikanaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli