Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni Kwa Maafisa Wanafunzi Shahada ya Sayansi ya Kijeshi (BMS) Maafisa wanafunzi Kundi la 05/21 na kundi la 71/23 Regular katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 28 Novemba, 2024.
Maafisa hao wapya wamekuwa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika cheo Cha Luteni USU ambapo kundi la 05/21 BMS lenye idadi 74 wamepata mafunzo katika chuo Cha Mafunzo ya kijeshi Monduli Kwa muda wa miaka mitatu na kuhitimu shahada ya Sayansi ya kijeshi.Aidha kundi la 71/23 Regular lenye idadi 95 Maafisa wapya wamepata mafunzo yao Kwa mwaka mmoja. Maafisa wapya idadi 88 wamepata mafunzo yao kutoka nchi rafiki za Afrika na nje ya bara la Afika.
Sherehe hizo za kamisheni na mahafali zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kijeshi akiwemo mhe.Dkt Stegomena Lawrence Tax,Waziri wa Ulinzi wa jeshi la kujenga Taifa,Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi Wastaafu, Makamanda, Majenerali Wastaafu wa JWTZ,Mhe.Paul Christian Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shem Kiswaga.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli